Home Unlabelled CHEKI HII ZAWADI YA BIRDMAN KWA BIEBER
CHEKI HII ZAWADI YA BIRDMAN KWA BIEBER
By burudanibuzz At April 08, 2014 0
Msanii ambaye siku za hivi karibuni amekuwa akikumbwa na skendo pamoja na matatizo mbalimbali Justin Bieber kupitia ukurasa wake wa Instagram amemshukuru bosi wa Young MOney Cash Money (YMCMB) Birdman kwa kumpa zawadi ya gari aina ya Bugatti Veyron Grand sport yenye thamani zaidi ya dola milioni moja. "Uncle Stunna luv. My first Bugatti #generosity." ndivyo alivyoandika Bieber huku Uncle stunna ikiwa ni jina la utani la msanii Birdman.
Birdman ni mpenzi wa magari ya kifahari na kila mwaka staa huyo inakadiriwa ananunua magari zaidi ya mia moaj. Bieber na Birdman wako studio wakiandaa baadhi ya nyimbo kwa ajili ya msanii huyo ambaye albamu yake ya Journals iliyotoka mwaka jana ilifanya poa sokoni.

