Home Unlabelled CHELSEA HIYOOOOOOOO NUSU FAINALI UEFA
CHELSEA HIYOOOOOOOO NUSU FAINALI UEFA
By burudanibuzz At April 08, 2014 0
Licha ya kufungwa 3-1 kwenye mchezo wa awali, Chelsea ya Jose Mourinho iliwaduwaza Paris Saint Germain kwa kuichapa 2-0 na kusonga mbele hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya (UEFA). Chelsea ikicheza darajani Stamford Bridge ilipata bao la kuongoza kupitia mchezaji wa kimataifa wa Ujerumani Andre Schurrle dakika ya 32 ya mchezo goli lililodumu mpaka dakika 3 kabla ya muda kwisha ambapo mchezaji aliyetokea benchi Demba Ba alipotia wavuni goli la pili lililowaondosha PSG kwa sheria ya mabao ya ugenini. Chelsea ilionekana kuwa na ari kuanzia dakika za mwanzo wa mchezo na walishambulia mara kwa mara japokuwa hawakufanikiwa kupata mabao mengi. Mshambuliaji wa PSG EdinsonCavani, alikosa mabao mengi ambayo yangeisaidia timu yake kuvuka kufikia nusu fainali kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo.