MILEY CYRUS TENA

Ana miaka 22 tu, followers zaidi ya milioni 17 twitter huku akiwa na utajiri unaokadiriwa kufikia dola milioni 150. Ni mwigizaji mzuri na pia mwanamuziki lakini haishiwi vituko kwa siku za hivi karibuni. Miley ni mtumiaji mzuri wa madawa ya kulevya hasa bangi huku pombe ikiwa ni moja kati ya starehe zake muhimu lakini ameendelea kuwika katika fani zake. Kwa sasa mwanadada huyo alikuwa na tour aliyoipa jina la Bangerz lakini taarifa zinasema kuwa hapo jana alishindwa kupanda jukwaani kutumbuiza katika tour hiyo Charlotte, North Carolina.Shoo hiyo ilifutwa dakika 30 tu kabla ya muda wa kuanza kwa madai kuwa msanii huyo alipata mafua na madaktari wakamuamuru kupumzika. Mashabiki waliojitokeza katika shoo hiyo watarudishiwa pesa zao. Kupitia mtandao wa twitter mashabiki wengi wamesikitishwa na kilichotokea na hizi ni baadhi ya tweets.
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates