KOMBE LA DUNIA 2022 KUTOFANYIKA JUNE

Jerome Volcke-Katibu mkuu FIFA
Utamaduni wa mashindano ya kombe la dunia kufanyika mwezi June hadi July umebadilishwa kwa ajili ya mashindano yatakayofanyika Quatar mwaka 2022. Katibu mkuu wa shirikisho la soka ulimwenguni (FIFA), Jerome Valcke amesema michuano hiyo inatarajiwa kufanyika kati ya Novemba na Januari 15 huku uamuzi wa kuhusu michuano hiyo ikisubiri kikao cha kamati kuu ya FIFA.
Uamuzi rasmi kuhusu kipindi cha kufanyika kwa mashindano hayo unatarajiwa baadae mwaka huu hasa baada ya mashindano ya kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil. Changamoto inayokumba mashindano hayo kutofanyika muda wake wa kawaida ni hali ya joto iliyokithiri nchini Quatar katika kipindi cha miezi ya June-July.

 Quatar inajiandaa kuwa mwenyeji wa michuano hiyo ambapo hoteli na viwanja vipya vinajengwa kwa kasi. Baadhi ya viwanja vya kuvutia vinavyotarajiwa kumalizika kabla ya mwaka 2022 kwa ajili ya mashindano hayo



Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates