Home Unlabelled CHELSEA WAMKOSA GUARIN
CHELSEA WAMKOSA GUARIN
By burudanibuzz At January 08, 2014 0
Juhudi za klabu ya Chelsea kusaka huduma za kiungo wa kimataifa wa Colombia anayekipiga Internazionale Milan, Fredy Guarin zimegonga ukuta baada ya klabu ya Inter kubadili mawazo ya kumpiga bei kiungo huyo. Inter Milan ilitangaza kumuuza Guarin kabla ya kuamua kumbakisha kwa mujibu wa tovuti ya klabu hiyo kupitia mkurugenzi wa Michezo Piero Ausilio. Tetesi zinasema usajili huo umeshindikana baada ya Chelsea kutofikia dau la Euro milioni 15 ambalo Inter Milan waliweka kama thamani ya kiungo huyo.