SABABU ZA ROONEY KUNG'ANG'ANIA KUONDOKA OT

HAMNIONI?????

DISAPPOINTED, HEARTBROKEN ROONEY
Mshambuliaji kiwango wa Manchester United
na timu ya taifa ya Uingereza Wayne Rooney ameendelea kusisitiza azma yake ya kuihama timu hiyo baada ya kuwepo Old Trafford kwa miaka 9. Mshambuliaji huyo aliyetua Man U kwa uhamisho wa paundi milioni 26 mwaka 2004 akitokea Everton, anahisi kutotendewa haki katika klabu hiyo. Kwa mujibu wa mtandao wa The Sun, hasira za Rooney zinachochewa na kitendo cha staa huyo kuchezeshwa nyuma wa Mholanzi Robin Van Persie.
Mpaka sasa Chelsea na baadhi ya klabu zingine kubwa ziko tayari kumsajili Rooney huku uongozi wa Manchester United ukiendelea kusisitiza kuwa mshambuliaji huyo hauzwi. 

Hii si mara ya kwanza kwa Rooney kutaka kuihama klabu hiyo kwani mwaka 2010 nusra aihame klabu hiyo huku mashabiki wakimshutumu na kumshambulia kipindi hicho. Hadi sasa haijajulikana kama klabu itakubali kumuuza au la lakini hali si shwari kati ya mshambuliaji huyo na timu.
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates