MADAWA, POMBE ZAMKATISHA MAISHA



Utumiaji wa pombe pamoja na madawa ya kulevya aina ya Heroine ndiyo chanzo cha kifo cha mwigizaji na mwanamuziki mwenye asili ya Canada Cory Monteith ripoti zimeeleza. Monteith aliyefariki tarehe 13 mwezi huu alijulikana kupitia mchezo wa runinga uliojulikana kama Glee uliokuwa ukirushwa na televisheni ya Fox. Muigizaji huyo ana historia ya utumizi wa madawa ya kulevya tangu alipokua na miaka 13 na baadaye alikimbia shule akiwa na miaka 16 tu.  Mwigizaji huyo amefariki akiwa na miaka 31 akiongeza wimbi la mastaa kupoteza maisha kutokana na
Cory kwenye moja ya scenes kwenye MONTE CARLO
matumizi ya madawa ya kulevya na pombe.
Monteith amepata tuzo tatu kutokana na kuigiza Glee huku akionekana kwenye zaidi ya michezo 20 ya televisheni. Kwa upande wa filamu Cory ameonekana kwenye filamu kama Monte Carlo akiwa na Selena Gomez, Katie Cassidy, Leighton Meeser na wengine wengi. Brothers & Sisters, Bloody Mary, Killer Bash, White Noise:The Light na The Invisible ni kati ya filamu nyingi alizoigiza Cory.
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates