MANDELA WA HOLLYWOOD

Huku hali ya afya  ya Rais wa kwanza mweusi na mwanaharakati dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini Nelson Mandela ikiendelea kuwa kizungumkuti, filamu inayomhusu mwanasiasa huyo nguli inatengenezwa. Mandela ambaye hapo kesho anatarajiwa kutimiza miaka 95 ameendelea kulazwa hospitalini huku taarifa zikisema kuwa afya yake haijatengemaa.
Mwigizaji huyo amedokeza kuwa, uhusika wa Mandela aliopewa kuigiza kwenye hiyo muvi ilikua kazi ngumu kutokana na ukubwa wa Mandela na ukweli kuwa wametumia kitabu bila kukutana na Mandela mwenyewe ambaye angewaongezea baadhi ya vitu ktk filamu hiyo. 
Idris Elba, mwigizaji mashuhuri kutoka Hollywood anaigiza kama Nelson Mandela katika muvi "Mandela: Long Walk To Freedom" ambayo imetokana na kitabu cha mwanasiasa huyo. Idris ambaye pia ni mwanamuziki ni moja kati ya waigizaji weusi bora kuwahi kutokea kwenye filamu nchini Marekani. Mwigizaji huyo amaeigiza zaidi ya 25 kati ya mwaka 1999 na mwaka huu 2013.
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates