

Katika hali isiyo ya kawaida jamaa mmoja ambaye alikuwa anajifunza udereva alipiga simu kuwataarifu watu wa Emergency kuwa mwalimu ambae anamfundisha kuendesha gari alichelewa kufika. Wahudumu wa simu ya dharura wamedokeza kuwa hii si mara ya kwanza wao kupokea simu za namna hiyo kwani mara nyingi watu wanapiga kuripoti kutopewa huduma hotelini na matukio mengine yasiyokuwa na umuhimu wala dharura.