TRUE LOVE????

BOB & BERNIE
Dunia in mambo na mapenzi ni jambo lisilotabirika. Kama kuna mtu ulikuwa unamzimia kuanzia utotoni labda ni wakati wako wa kukaa na kusubiri kuona kama mtakutana tena.  What is yours will always be yours. Nchini Uingereza Bob Humphries mwenye miaka 89 na  Bernie Bluett miaka 88 wapo katika mipango ya kufunga ndoa.  Wananfoa hao watarajiwa walikutana kwa mara ya mwisho Bob alipokuwa na miaka 18 huku Bernie alikuwa na miaka 17 tu. Baada ya kutoonana kwa takriban miaka 70, wawili hao walikutana tena mwaka 2011 na tangu hapo wamekuwa pamoja. Bob amesema kuwa tangu akutane na mwanamke huyo miaka 70 iliyopita ameendelea kumpenda na walipokutana ndipo mipango ya kuoana ilianza. Wawili hao walitengana kipindi cha vita kuu ya pili ambapo baadaye kila mmoja alijikuta kwnye ndoa nyingine.


Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates