Mshambuliaji wa Manchester City raia wa Argentina Carlos Tevez amekamilisha uhamisho wake kwenda Juventus ya Italia kwa ada ya uhamisho inayokadiriwa kufikia pauni milioni 10. Tevez alisajiliwa na Man City akitokea Man United mwaka 2009 kwa gharama zinazokadiriwa kufikia pauni milioni 47 japo miak yake Etihad haikuwa a mafnikio sana. Mchezaji huyo amekabidhiwa jezi namba 10 ambayo ilitumiwa na mkongwe wa Juve mwenye heshima kibao Alessandro Del Piero. Tevez ambaye pia alikua anahitajika AC Milan amesema uamuzi wake wa kuhamia Juve umetokana na suala la Juve kumhitaji zaidi ya AC Milan.
Home Unlabelled TEVEZ ATUA JUVENTUS