Timu ya taifa ya Spain inayoshikilia taji la Kombe la dunia na lile la EURO wameendelea kuthibitisha ubora wao baada ya kushinda magoli 10-0 dhidi ya timu ngeni mabingwa wa Oceania Tahiti. Mshambuliaji wa Chelsea Fernando Torres alifunga magoli manne dakika za 5, 33, 57, 78. David Villa alifunga magoli matatu kwenye ushindi huo wa kihistoria huku David Silva akiongeza mengine mawili na baadaye Juan Mata akafunga moja.
Wawakilishi wa Afrika timu ya Nigeria katika mchezo mwingine walishindwa kutamba mbele ya Uruguay baada ya kutandikwa 2-1 matokeo yanayoiweka Nigeria kwenye nafasi finyu kufuzu kwa hatua inayofuata. Kiungo mwenye ukame wa magoli John Obi Mikel ndiye aliyefunga goli la Nigeria wakati magoli ya Uruguay yalipatikana kupitia Lugano na Diego Forlan. Nigeria inabidi ishinde mechi yake dhidi ya Hispania huku ikiomba Uruguay wafungwe au watoke sare na vibonde Tahiti au wapate sare na matokeao ya Uruguay yakiwa ni kufungwa jambo linaloonekana kutokua na uwezekano. Kwa ubora wa Uruguay, kufungwa ba timu ambayo ishafungwa magoli 16 kwa mechi mbili inaweza kuwa si jambo la kwaida na hali hii inaipa Nigeria hali ngumu zaidi.