BRAZIL, ITALY ZASONGA MBELE MICHUANO YA MABARA




BALLO KAZIN

NEYMAR
Mabingwa wa dunia mwaka 2010, Italia na wenyeji wa michuano ya mabara ambao pia watakua wenyeji wa kombe la dunia mwaka 2014 Brazil wamepata nafasi ya kusonga mbele kwenye michuano ya Mabara baada ya kushinda mechi zao. Brazil ikicheza nyumbani ikiwa na nyota wake wengi akina Neymar, wamewafunga Mexico 2-0 na kijikatia tiketi ya Nusu fainali huku Italia ikitoka nyuma na kushinda mchezo dhidi ya Japan. Mpaka dakika ya 40 ya mchezo kati ya Japan na Italia, Japan ilikua ikiongoza kwa magoli 2-0. Magoli ya Japan yalifungwa na Honda dakika ya 21 huku Shinji Kagawa akiipa Japan bao la pili. Daniel De Rossi aliifungia Italia goli la kwanza dakika ya 41 kabla ya beki wa Japan Uchida kujifunga dakika ya 50. Mchezaji wa AC Milan alifunga kwa penalti dakika ya 52 kuifanya Italia iwe mbele kwa 3-2 kabla ya Okazaki kuisawashia Japan dakika ya 69. Giovinco alimaliza ubishi wa mechi hiyo baada ya kufunga goli la nne na la mwisho katika mechi hiyo dakika nne kabla ya mchezo kumalizika. 
Katika mechi nyingine, wenyeji Brazil waliifunga Mexico 2-0 kwa msaada wa Neymar pamoja na Jo' dakika ya 9 na 93. Katika mechi hiyo iliyochezwa Estadio Castelao, Brazil ilijihakikishia nafasi ya kucheza nusu fainali ikisubiri mechi ya mwisho dhidi ya Italia itakayoamua ni timu ipi inakuwa ya kwanza katika kundi A.  Mara ya mwisho kombe la Mabara (Confederations Cup) lilibebwa na Brazil, hii ilikuwa ni mwaka 2009 nchini Afrika Kusini.
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates