ANDY CARROLL ATUA RASMI WEST HAM


Mshambuliaji wa aliyenunuliwa Liverpool kwa ada ya pauni Milioni 35 kutoka Newcastle mwaka 2011 amesaini mkataba wa miaka sita kuichezea West Ham United. Carroll amesaini mkataba huo kuichezea ti,u ambayo msimu uliopita aliichezea kwa mkopo baada ya kuwa na msimu mbaya sana Liverpool. Uhamisho huo umeigharimu The Hammers kiasi cha pauni milioni 19 huku Carroll akitarajia kupata mshahara wa pauni Laki moja kwa wiki. Akizungumza baada ya kusaini Carroll ameonesha kufurahishwa kwake na hatua hiyo huku akielezea matarajio ya kufanya vema kama msimu uliopita “It’s fantastic for me to be here. I really enjoyed last season, and that shows in me coming back and making it permanent."
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates