Timu ya taifa ya Brazil iliichapa Uruguay 2-1 kujikatia tiketi ya fainali ya kombe la mabara. Diego Forlan alikosa penalti dakika ya 22 ya mchezo kabla ya Fred kuifungia Brazil bao la kuongoza dakika ya 41 kabla ya na mshambuliaji Edinson Cavani kuisawazishia Uruguay dakika ya 48. Paulinho ndiye aliyewapa Brazil tabasamu la siku baada ya kufunga bao la ushindi dakika nne kabla mchezo kwisha.
Hii inakuwa ni mara ya tatu mfululizo kwa Brazil kucheza fainali ya Mabara na safari hii inasubiri mshindi kati ya Italia na Hispania ili kujua itacheza na timu gani fainali. . Uruguay haijawahi kuishinda Brazil kwa takriban miaka 20 sasa na ushindi wa jana umeongezea ubabe walionao Brazil dhidi ya timu hiyo.