BRAZIL MABINGWA MABARA





Kinyume na matarajio ya wengi, timu ya taifa ya Hispania hapo jana ilitandikwa 3-0 na wenyeji wa michuano ya kombe la mabara Brazil ambao pia watakua wenyeji wa michuano ya kombe la dunia hapo mwakani. Brazil wakicheza mbele ya mashabiki maelfu kwenye uwanja wa Maracana walifanikiwa kupata bao la kuongoza kupitia kwa Fred dakika ya pili ya mchezo kabla ya mshambuliaji mpya wa Barcelona Neymar kuongeza bao jingine dakika ya 44. Brazil walijihakikishia ushindi huku Hispania ikibaki na aibu dakika ya 47 ambapo Fred kwa mara nyingine alitia mpira wavuni na kukata matumaini ya Hispania kubeba taji lao la tatu ndani ya miaka mitatu. Laiti kama wangeshinda, Hispania ngejiwekea rekodi ya kipekee kwa kubeba mataji yote iliyoshiriki kwani timu hiyo inashikilia mataji mawili kwa sasa, Kombe la dunia pamoja na lile la Ulaya. Gerard Pique alioneshwa kadi nyekundu dakika ya 68 ya mchezo na kuwaacha Hispania wakiwa pungufu.Mchezaji aliyefunga penalti ya mwisho kuivusha Hispania kuingia fainali, Jesus Navas aliwapa mikikimikiki mabeki wa Brazil na kufanikiwa kupata penalti ambayo hata hivyo haikuzaa matunda baada ya Sergio Ramos kushindwa kuutia mpira kimiani.


Mchezaji wa brazil Neymar amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa michuano nyuma yake kukiwa na Andres Iniesta na Paulinho. Tuzo ya mfungaji bora imeenda kwa Fernando Torres, kipa bora Julio Cesar na fair play imechukuliwa na Hispania.









Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates