BRAZIL, ENGLAND HAKUNA MBABE

CHAMBERLAIN & ROONEY



Timu ya taifa ya Brazil jana imeshindwa kutamba nyumbani kwenye uwanja wa kihistoria wa Maracana baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 na timu ya taifa ya Uingereza "Three Lions. Fred na Paulinho walifunga magoli ya Brazil dakika ya 57 na 82 huku England wakipata magoli yao kupitia kwa Alex Oxlade-Chamberlain na Wayne Rooney. Mechi hiyo ni ya kwanza kuchezwa kwenye uwanja huo baada ya kufanyiwa marekebisho. Uwanja huo ni moja kati ya viwanja vyenye mvuto na kilitumika kwenye fainali za kombe la dunia mwaka 1950. Uwanja huo pia utatumika kwenye fainali zijazo za kombe la dunia 2014,
pamoja na kombe la mabara mwezi huu wa June.
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates