R.I.P NGWEA |
Mwili wa msanii Albert Mangwea unaweza kufika Dar es salaam
leo jioni au kesho asubuhi kutokana na taarifa zilizotoka Afrika Kusini. Ngwea
alifariki May28 siku ya Jumanne iliyopita na taratibu zinafanyika ili
kuusafirishi mwili wake kwa ajili ya kuwapa mashabiki na Watanzania nafasi ya
kumuaga msanii huyo ambaye kwa takribani miaka kumi amekuwepo kwenye anga la
muziki wa kizazi kipya. Taarifa zinasema kuwa u balozi wa Tanzania nchini
Afrika Kusini kwa sasa unashughulikia cheti cha kifo pamoja na nyaraka zingine
kabla ya kuusafirisha mwili huo.