KIPENZI CHA MASHABIKI |
Baada ya uongozi wa Real Madrid kutangaza kuachana na kocha mkuu wa timu hiyo Jose Mourinho na kuanza mchakato wa kumpata kocha mwingine, kocha huyo wa zamani wa Porto, Chelsea na Inter Milan inasemekana yuko mbioni kuingia mkataba na timu yake ya zamani Chelsea. Morinho maarufu kama 'The Special One' aliondoka Chelsea mwaka 2007 baada ya kukosa maelewano mazuri na uongozi wa juu Chelsea. Kocha huyo ambaye msimu huu hakufanikiwa kunyakua walau kombe moja anasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Chelsea ambao wanampenda sana kocha huyo. Suala la Mourinho kuhamia timu nyingine lilitokana na mwenendo wa timu yake pamoja na jinsi vyombo mbalimbali vya habari pamoja na wachambuzi kadhaa walivyokuwa wakimwandama kocha huyo hivyo kuona hapendwi na watu wa Hispania. Tayari wachezaji wengi wa Chelsea wameelezea matumaini yao makubwa endapo kocha huyo akijiunga na mabingwa hao wa EUFA-Europa league. Mshambuliaji wa Chelsea, Fernando Torrea amesema "The chance to work with Mourinho is something every player want to do atleast once in their lives"