TONTO DIKEH KUIWAKILISHA NIGERIA BIG BROTHER

     

Inaonekana kama Big Brother shindano linalofanyika kila mwaka kule Afrika Kusini linabadilika kuwa shindano la mastaa baada ya kuwepo tetesi  kuwa mwanadada staa wa movie Nigeria Tonto Dikeh ndiye atakayeiwakilisha Nigeria. Tonto mwenye vituko lukuki ni mwigizaji mwenye jina kubwa sehemu nyingi Afrika kutokana na umahiri wake wa kuigiza huku siku za hivi karibuni akijihusisha na muziki. Mwanadada huyo ambaye amekuwa akituhumiwa kubadili la rangi ya mgozi yake a.k.a kujichubua ana miaka 28 na ameshiriki filamu nyingi kama Tea or Coffee, Away match, Games fools play,The plain truth, Love my way na nyingine nyingi huku wimbo wake unaojulikana kama Jeje uki-hit poa kwenye radio mbalimbali.
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates