MULLER, ROBBEN & GOMEZ WAIUA BARCA

MULLER & ROBBEN
THOMAS MULLER NA WENZAKE WAKISHANGILIA
JORDI ROURA
Barcelona ikicheza kwenye uwanja wa Allianz Arena ilichapwa 4-0 na wenyeji wao katika mechi kwanza ya nusu fainal ya klabu bingwa Ulaya  (UEFA). Matokeo ya mechi hiyo hayakutarajiwa kutokana na uwezo mkubwa wa  Barcelona ambao wan mchezaji bora wa dunia mara nne Lionel Messi. Thomas Muller alifunga magoli mawili dakika ya 25 na 82, Mario Gomez alifunga dakika ya 49 huku mchezaji wa zamani wa Real Madrid na Chelsea Arjen Robben akifunga dakiaka ya 73. Lionel Messi ndiye alikua gumzo baada ya mechi ikitokana na ukweli kuwa staa huyo wa Argetina hakufanya jambo lolote la ajabu katika mechi hiyo kama watu wengi walivyotarajia. Messi ambaye wiki chache zilizopita alikuwa majeruhi alishindwa kabisa kuitingisha Bayern ambao walikuwa na morali ya ushindi. Mara baada ya mechi Arjen Robben alisema kuwa wanahitaji kufanya kazi kubwa zaidi ya jana ili kujisogeza kwenye fainali ya UEFA. Nae kocha msaidizi wa Barcelona Jordi Roura amedai kuwa jambo la kukata tamaa kwao halipo llicha ya kufungwa magoli mengi.

Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates