Home Unlabelled SITAOMBA USHAURI WA GUARDIOLA- HEYNCKES
SITAOMBA USHAURI WA GUARDIOLA- HEYNCKES
By burudanibuzz At April 13, 2013 0
Kocha wa Bayern Munich Jupp Heynckes ambae timu yake itapambana na Barcelona kwenye nusu fainali ya UEFA amesema kwamba hatamuomba kocha wa zamani wa Barcelona ambaye anajiandaa kuinoa Bayern kuanzia June, Pep Guardiola. Guardiola ni kocha ambaye kwa kiasi kikubwa anaifahamu Barca huku ikisemekana ndio chachu ya nyota kama Messi kufanya vizuri. Bayern na Barcelona zitakutana katika nusu fainali ya kwanza Allianz Arena Aprili 23 na mechi ya marejeano kuchezwa Aprili 30. Heynckes amesema haitaji ushauri wa Guardiola katika mechi hiyo. Kocha huyo ameweka wazi kuwa uwezo wake wa kufundisha ndio utawavusha na yeye hapokei ushauri kutoka kwa watu wengine.