REEBOK YAMTEMESHA ROZAY

ROZAY NA MOJA YA VIATU VYA REEBOK


Rapa mwenye mwili mkubwa na mashairi ya kutosha kutoka Miami ambaye pia anawakilisha Maybach Music Group MMG, Rick Ross a.k.a Rozay amejikuta akipoteza dili la matangazo baada ya kampuni ya Reebok kuamua kuvunja mkataba. Kama ilivyo kawaida ya kampuni kubwa duniani, suala la Rick Ross ku-rap mistari inayotafsiriwa kuunga mkono suala la ubakaji. Katika wimbo wa Rocko unaoitwa YOU DON'T EVEN KNOW (U.O.E.N.O), Rick amerap "Put molly all in her champagne, she ain't even know it",na kuendelea "I took her home and I enjoyed that, she ain't even know it.". Molly (MDMA) ni dawa inayotumika kupunguza maumivu ambayo wabakaji wengi hutumia kuwafanya mabinti wasiumie na tendo hilo hivyo kuwapa nafasi ya kufanikisha tendo hilo haramu la ubakaji. Baada ya Reebok kutangaza uamuzi wao rapa Rick Ross amejitokeza na kuomba radhi kwa mistari yake huku akiitakia Reebok mafanikio.
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates