NI MADRID VS DORTMUND, BARCA VS BAYERN NUSU FAINALI UEFA

   






Shirikisho la soka Ulaya (UEFA) limetoa ratiba ya nusu fainali ya michuano ya klabu bingwa ulaya ambapo Real Madrid ya Jose Mourinho itakuwa na shughuli pevu mbele ya Borussia Dortmund ya Ujerumani. Borussia ilikuwa kundi moja na Madrid na haikufungwa n Real hata mechi moja kati ya mbili walizocheza huku ikishikilia rekodi ya timu pekee ambayo haijashindwa hata mechi moja mpaka sasa. Bayern Munich walioitoa Juventus Turin watakua na kibarua kigumu mbele ya mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich. Bayern alikosa ubingwa mwaka jana mbele ya Chelsea na kocha wa Bayern Jepp Heynckes atataka kuipa Bayern ubingwa wa Ulaya kabla ya kumpisha kocha mpya wa klabu hiyo Pep Guardiola. Barcelona na Madrid zitaanza mechi zao ugenini jambo litakalowapa nafasi nzuri ya kusonga mbele dhidi ya timu hizo za Ujerumani.Barca wataifuata Bayern Allianz Arena tarehe 23 April kabla ya kucheza mechi ya marudiano Aprili 30 Camp Nou. Ratiba hiyo inafanana na ile ya mechi kati ya Madrid na Borussia Dortmund.

Katika UEFA Europa League, Chelsea itakutanna na wababe wa Manchester United FC Basel huku Benfica ya Ureno ikikipiga na Fenerbahce ya Uturuki. Mechi ya kwanza ya EUROPA league itachezwa Aprili 25 na mechi ya marudiano kuchezwa May 2.
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates