Msanii wa kundi la muziki kutoka Nigeria "P-SQUARE" Paul Okoye pamoja na mpenzi wake wa siku nyingi Anita wamefanikiwa kupata mtoto wa kiume waliyembatiza jina la Andre. Anita amejifungua salama mtoto huyo Atlanta nchini Marekani ambako P-Square wanaishi kwa sasa. Mapema mwaka huu memba mwingine wa kundi hilo Peter alifanikiwa kupata mtoto wa pili na mpenzi wake anayefahamika kama Lola Omatayo.