LEWANDOWSKI |
Safari ya timu mbili kubwa za ligi kuu Hispania nchini Ujerumani zimeishia pabaya baada ya jana Real Madrid kushindwa kufurukuta mbele ya Dortmund. Real Madrid ilifungwa 4-1 katika mechi hiyo huku mshambuliaji wa kimataifa wa Poland Robert Lewandowski akiibuka shujaa kwa kupachika magoli yote manne. Goli la Real Madrid lilifungwa dakika ya 43 na Cristiano Ronaldo lakinihalikutosha kuizuia timu ya Borussia Dortmund kufanya vyema na kujiweka katika nafasi nzuri ya kuingia fainali za UEFA zitakazopigwa uwanja wa Wembley mwezi May. Real Madrid kwa sasa inatakiwa kuifunga Dortmund 3-0 kwenye mechi ya marudiano ili iweze kufuzu kuingia fainali. Madrid ikitolewa UEFA itakua imebakiza matumaini ya kunyakua kombe la mfalme Copa Del Ray tu kutokana na tofauti za pointi kati yake na Barcelona wanaoongoza La Liga kwa sasa