"CANNIBAL" AFUNGIWA MECHI 10

TUKIO LA 2011
Mshambuliaji wa Liverpool raia wa Uruguay Luis Suarez "Cannibal" amefungiwa kucheza mechi 10 baada ya tukio la kumng'ata beki wa Chelsea Branislav Ivanovic katika mechi dhidi ya timu hizo mbili iliyochezwa jumapili Anfield. Kufungiwa kwa Suarez ni pigo kwa Liverpool inayomtegemea sana mshambuliaji huyo na kwa upande mwingine ndoto za mchezaji huyo kuchukua tuzo ya mfungaji bora wa ligi kuu Uingereza zimeyeyuka. Suarez mwenye magoli 23 yuko nyuma ya Robin Van Persis kwa goli 1 na ataanza kukosa mechi dhidi ya Newcastle jumamosi. Adhabu ya kwanza ilikuwa kusimamishwa mechi tatu lakini baadaye ilibadilishwa baada ya kuonekana adhabu ndogo. Hili si tukio la kwanza kwa Luis Suarez kung'ata kwani akiwa Ajax alishawahi kufungiwa mechi 7 kwa kosa kama hilo. Akiwa Ajax Suarez alimng'ata Otman Bakkal wa PSV Eindhoven mwaka 2011.
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates