VS
Siku chache baada ya kutweet madongo kwa radio ya Clouds FM, mwanamuziki wa longtime Judith Wmbura anayeibeba bongo flava kwa upande wa akina dada ametweet kuhusu ishu nyingine ambayo inawahusu waimbaji wawili wanaofanya poa Ben Pol na Linah. Jay Dee amedai kuwa wasanii hao hawakutokea kwenye shoo ambayo ilitakiwa ifanyike Nyumbani Lounge (Inamilikiwa na Jay Dee) licha ya kulamba advance kwa ajili ya shoo hiyo. Jide amedai wasanii hao yaani Lina na Ben Pol hawakutokea kwenye shoo kwa kuwa WALIKATAZWA. Twitter na BBM zimekua sehemu za malumbano kwa baadhi ya wasanii huku tukio la Jay Dee VS Ben Pol kikija wiki chache baada ya Ney kumporomoshea Nikki Mbishi matusi kupitia BBM. Ben Pol anaesemekana kuwa mmoja kati ya wasanii wastaarabu amemjibu Jay Dee huku akiuliza
Baada ya Ben Pol kutweet mara kadhaa msanii mwingine Rama D alitweet akionesha kumsapoti Ben Pol..........
Je tabia ya wasanii kugombana kupitia mitandao ya kijamii inamaanisha nini na itafikia wapi?????