SUMATRA YAPANDISHA NAULI

Mamlaka ya usafiri wa majini na nchi kavu SUMATRA imepandisha gharama za usafiri kwa mabasi yaendayo mikoani, daladala pamoja na vyombo vya majini. Viwango hivyo vipya vinatarajiwa kuanza kutumika Aprili 12 mwaka huu. Viwango vya nauli za Daladala vimeongezeka kwa Wastani wa asilimia 24.46 na mabasi ya masafa marefu vimeongezeka kwa asilimia 20.3 kwa mabasi ya kawaida, asilimia 16.9 kwa mabasi ya daraja la kati na asilimia 13.2 kwa mabasi ya daraja la juu. Kwa mantiki hiyo kiwango cha chini cha nauli kwa Daladala itakuwa shilingi 400 kwa umbali wa kilomita 10 na cha juu kikiwa ni shilingi 750 kwa umbali wa kilomita 26 hadi 30 huku Mwanafunzi akitakiwa kulipa nusu ya nauli ya mtu mzima shilingi 200. 

Kwa upande wa huduma ya Usafirishaji wa abiria kwa njia ya Reli ya Kati  viwango vya nauli vimepanda kwa asilimia 25 kwa Daraja la Kwanza na la Pili na asilimia 44.1 kwa daraja la tatu.
SUMATRA imeridhia kupandisha viwango vya nauli baada ya kupitia maombi yaliyowasilishwa na Wamiliki wa Mabasi ya Masafa marefu, Daladala pamoja na yale yaliyowasilishwa na Shirika la Reli nchini (TRL) likipendekeza kupitia upya viwango vya nauli.
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates