JAGUAR ANUNUA NDEGE BINAFSI

AIR JAGUAR
Tumezoea kusikia wasanii wa Marekani akina Jay Z, P Diddy, Rick Ross, AKON na wengine kumiliki ndege, boti na vyombo vingine vya thamani huku Afrika Mashariki ishu kubwa ikiwa ni magari. Kwa mara ya kwanza Afrika Mashariki imepata msanii wa kwanza ambae ana ndege binafsi ukiachana na Prezzo ambaye mwanzoni alisemekana kumiliki ndege. Aliyekua adui wa Prezzo msanii Jaguar anayetamba na ngoma mpya aliyoipa jina kipepeo ndiye msanii pekee mwenye ndege Afrika Mashariki. Jaguar ni mfanyabiashara mkubwa huku akisemekana kuwa moja kati ya wasanii wenye mkwanja mrefu zaidi Mashariki mwa Afrika. Msanii huyo pian anafahamika kwa ukaribu wake na rais wa sasa wa Kenya Mh. Uhuru Kenyatta na wanasiasa wengine maarufu nchini humo akiwemo aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga.



Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates