Goli la David Luiz dakika ya 4 za nyongeza kabla ya mechi kwisha iliipa timu ya Chelsea matumaini ya kuingia fainali ya EUFA EUROPA league baada ya kushinda 2-1 dhidi ya FC Basel. Wakiwa nyumbani St. Jacob Park FC Basel walianza vibaya baada ya wageni wao Chelsea kupata goli la kuongoza kupitia kwa Victor Moses dakika ya 12 ya mchezo. Hata hivyo penalti iliyolalamikiwa sana na Chelsea pamoja na kocha wao wa muda Rafael Benitez dakika ya 87 ya mchezo iliipa Basel bao la kusawazisha kabla ya David Luiz kuzima ndoto za Basel kutoa sare kwa mpira wa adhabu aliopiga dakika ya mwisho ya muda wa nyongeza. David Luiz ambaye hiyo jana alipangwa kucheza nafasi ya kiungo mkabaji badala ya beki kama alivyozoeleka alicheza vyema kwenye hiyo mechi. Kwa matokeo hayo chelsea inahitaji ushindi au are ya aina yoyote ili itinge fainali ambapo itakutana na Fenerbahce au Benfica. Katika mechi ya nusu fainali nyingine Fenerbahce ikiwa nyumbani ilifanikiwa kuifunga Benfica ya Ureno na hivyo kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kuingia fainali. Fainali za EUFA EUROPA League msimu huu zitafanyika May 15 mjini Amsterdam Uholanzi.