DORTMUND HIYOOOOOO FAINALI

Borussia Dortmund licha ya kufungwa 2-0na Real Madrid pale Santiago Bernabue imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya UEFA kwa uwiano wa 4-3 kutokana na ushindi wa 4-1 walioupata nyumbani Ujerumani. Ilibidi Madris wasubiri haadi dakika ya 82 kupata bao la kuongoza lililofungwa na mlinzi na kapteni wao Sergio Ramos huku mfaransa Karim Benzema akiongeza bao la pili dakika ya 88 ya mchezo. Kwa maana hiyo Dortmund inasubiri kujua timu itakayocheza nayo fainali kati ya Barcelona wenye nafasi finyu na Wajerumani wenzao Bayern Munich. Barcelona watakua Nou Camp usiku huu kujaribu kufanya maajabu dhidi ya Bayern baada ya mechi ya mzunguko wa kwanza kumalizika kwa Barca kutandikwa 4-0 hivyo itawabidi kutumia nguvu za ziada kuhakikisha wanashinda 5-0 ili kusonga mbele.
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates