BARCA AIBU

Barcelona mabingwa watarajiwa wa La Liga na washindi wa UEFA 2010-2011  hapo jana walichapwa 3-0 na Bayern Munich na kutolewa kwenye hatua ya nusu fainali ya UEFA kwa jumla ya 7-0 na kuandika historia ya aibu ambayo imeshangaza ulimwengu. Wakicheza bila nyota wao Lionel Messi mbele ya mashabiki wao Nou Camp Barca walishindwa kupata walau goli moja na kuwapa vijana wa Heynckes ushindi huo wa kihistoria. Arjen Robben alifunga goli la kwanza dakika ya 48 kbla ya Gerard Pique kujifunga na Thomas Muller kumalizia ushindi huo muhimu ambao umewahakikishia nafasi ya fainali dhidi ya Borussia Dormund pale Wembley May 25.
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates