BALE BORA KWA MWAKA

SUAREZ & BALE

Shirikisho la wachezaji wa kulipwa (Professional Footballers Association-PFA) imemtunuku Gareth Bale wa Tottenham kuwa mchezaji bora wa kulipwa kwa msimu wa 2012-2013. Bale ambaye kwa kiasi kikubwa amechangia matokeo mazuri ya Tottenham kwa kufunga magoli 19 ameshinda akimwacha mchezaji mwingine aliyebeba timu mgongoni Luis Suarez wa Liverpool. Suarez mwenye magoli 23 amejitutumua msimu huu na kuifanya Liverpool kufika nafasi ya saba ya msimamo wa ligi. Gareth
Bale baada ya kupata tuzo alisema "It's a massive honour. To be voted by your peers is one of the biggest things in the game. It's great to win it and I am delighted," Bale amekuwa gumzo huku timu ya Real Madrid ikitoa tamko la kumhitaji wakati
Manchester United, Barcelona na timu zingine kubwa zikihitaji huduma ya nyota huyo wa Wales. Gareth Bale pia amenyakua tuzo ya mchezaji chipukizi aliyefanya vizuri kwa msimu huu.
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates