UHURU KIDEDEA

UHURU KENYATTA--RAIS WA 4 KENYA
Licha ya wachambuzi wengi wa masuala ya siasa kutabiri kuwa Raila Odinga ndiye angeshinda kura za urais mambo yameenda kinyume baada ya wnanchi wa Kenya kuamua Uhuru Kenyatta mtoto wa rais wa kwanza wa Kenya kutangazwa kuwa mshindi hivyo kuwa rais wa nne wa Jamhuri ya Kenya. Uhuru ambaye ana kesi kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC ameshinda kwa zaidi ya asilimia 50 jambo linalofanya kutokuwepo kwa duru ya pili ya uchaguzi. Waangalizi wa kimataifa wamedai kwamba uchaguzi huo ulikuwa wa huru na haki japo mgombea aliyeshindwa bwana Raila Odinga anadai kuibiwa kura zake. Zoezi zima la uchaguzi limefanyika katika njia ya amani huku Wakenya wakiwa wameapa kutorudia makosa waliyofanya 2007 na kuleta umwagikaji wa damu.
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates