MAN UNITED -----------------------------------

CR 7
Mashetani wekundu wameyaaaga rasmi mashindano ya klabu bingwa ulaya baada ya kunawishwa na Real Madrid. Baada ya kupata sare ya 1-1 dhidi ya Madrd kule Santiago Bernabue, Manchester United walikuwa na matarajio makubwa kusonga mbele lakini vijana wa kocha mwenye maneno mengi Jose Mourinho waliamua vingine. Man U ilifungwa 2-1 nyumbani Old Trafford. Kiungo mwenye asili ya Ureno alionyeshwa kadi nyekundu jambo ambalo kwa mujibu wa jose mourinho lilichangia ushindi wao. Wachezaji wawili ambao walikuwa ligi kuu ya Uingereza kabla ya kuhamia Madrid, Luka Modric na Cristiano Ronaldo ndio waliopeleka kilio Old Trafford huku Man U wakiambulia goli la kujifunga la beki Sergio Ramos
. Katika mechi nyingine Borussia Dortmund waliitandika Shakhtar Donetsk 3-0 na kuingia hatua ya 8 bora.
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates