HUGO CHAVEZ AFARIKI DUNIA

CHAVEZ
Aliyekuwa rais wa Venezuela bwana Hugo Chavez hatimaye amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 58 nchini Cuba alipokuwa akiendelea na matibabu ya ugonjwa wa kansa. Taarifa zilizotoka jana zilisema kwamba rais huyo alikuwa na matatizo kwenye mfumo wa upumuaji baada ya operesheni na mpaka hiyo jana hali yake haikuwa nzuri.Chavez amekuwa rais wa Venezuela kuanzia mwaka 1999 na msimamo wake dhidi ya Marekani na nchi zinazoisapoti Marekani umempa umaarufu mkubwa duniani. Pamoja na kuongoza kwa muda mrefu raia wengi wa Venezuela hawakuwa na matatizo makubwa na kiongozi wao huyo. Makamu wa Rais wa Venezuela Nicolas Maduro atashikilia madaraka kwa muda ambapo uchaguzi unasemekana utafanyika baada ya siku 30. Viongozi mbalimbali duniani akiwemo rais wa Marekani Barack Obama ametuma salamu za rambirambi kwa wananchi wa Venezuela. Mwili wa Chavez unatarajiwa kuzikwa siku ya ijumaa.
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates