TOTTENHAM YASIMAMISHWA

SUPER FRANKIE
Tottenham Hotspurs baada ya kufuzu kuingia hatua ya nane bora kwa mbinde dhidi ya Inter Milan hapoa jana iliingia mkenge baada ya kuchapwa 1-0 na Fulham. Mshambuliaji wa zamani wa Tottenham na Manchester Dimitar Berbatov alifunga bao la pekee kwenye mechi hiyo ambapo kwa matokeo hayo Tottenham inashika nafasi ya nne nyuma ya Chelsea ambayo jana ilishinda 2-0 dhidi ya West Ham na kujisogeza nafasi ya 3. Frank Lampard alikaribia kuvunja rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote Chelsea kama angetumia nafasi nzuri alizopata. Newcastle ilifungwa 2-1 licha ya kufuzu nane bora Europa. Aruna Kone alitia msumari wa mwisho kwenye jeneza la Newcastle dakika ya 90
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates