Home Unlabelled BARCA YACHAPWA TENA
BARCA YACHAPWA TENA
By burudanibuzz At March 02, 2013 0
Jose Mourinho kwa mara nyingine ameibuka na ushindi dhidi ya timu hasimu Barcelona. Pamoja na Barca kuendelea kuongoza La Liga raha ya uongozi wa ligi imepotea kutokana na matokeo ya mechi hiyo ikizingatiwa kuwa ndani ya wiki moja wamefungwa mara mbili na Madrid. Cristiano Ronaldo, Sami Khedira, Mesut Ozil, Higuain na Alvaro Arbeloa walianzia benchi jambo lililowashangaza watu wengi. Lionel Messi alifunga goli la Barcelona huku nahodha wa Madrid kwa sasa Sergio Ramos na Karim Benzema wakifunga magoli ya Real Madrid.