KAGAWA, SUAREZ WAPIGA HAT TRICK

Kiungo wa Man United Shinji Kagawa  alifunga magoli matatu kwenye ushindi wa 4-0 dhidi ya Norwich. Wayne Rooney alifunga bao la mwisho dakika ya 90 na kuipa Man United pointi zote tatu. Manchester inaendelea kuongoza msimamo wa ligi kuu huku jirani zao Manchester City wakiwa katika nafasi ya pili. Hat trick nyingine ilikuwa ya mkali kutoka Uruguay anayekipiga Liverpool, Luis Suarez ambaye aliisaidia timu yake kuibuka na ushindi dhidi ya Wigan Athletic. Wigan kwa sasa iko nafasi ya 17 na Liverpool inashika nafasi ya 8 kwenye msimamo wa ligi
Chelsea ilijitutumua na kupata ushindi mwembamba wa goli 1-0 dhidi ya West Bromwich na kuwapa matumaini ya kuendelea kuwemo top four. Hata hivyo Chelsea wanaiombea mabaya Tottenham  ifungwe na Arsenal hii leo ili waendelee kubaki katika nafasi ya tatu kwani ushindi wa Tottenham utawashusha hadi nafasi ya nne karibu na Arsenal ambayo ikishindwa mechi ya leo itaendelea kubaki nafasi ya tano.
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates