Mambo si mambo Zanzibar baada ya kuwepo kwa matukio mengi yanayoleta mtafaruku baina ya Waislamu na Wakristo. Siku chache baada ya kuuwawa kwa padre Evarist Mushi hapo jana tukio kulitokea tukio la kanisa la Pool of Siloam kuchomwa moto. Tukio hilo ni moja ya matukio ya hivi karibuni yanayoongeza hofu miongoni mwa Watanzania wapenda amani. Kutokana na matukio hayo jeshi la polisi limeamua kuanza utaratibu wa kulinda makanisa ili kuepusha matukio mengine mabaya kwenye makanisa hayo