ARSENAL CHALI KWA BAYERN

KROOS AKISHANGILIA 
Timu ya soka ya Arsenal maarufu kama THE GUNNERS jana usiku walikiona cha moto baada ya kuchapwa 3-1 na Bayern Munchen. Arsenal ilishindwa kutumia vema uwanja wake wa nyumbani wa Emirates na kuwapa Bayern ushindi huo ambao unaipa Arsenal nafasi finyu ya kusonga mbele katika michuano ya UEFA. Bayern inahitaji sare ya aina yoyote nyumbani Allianz Arena  kutinga hatua ya nane bora. Mabao ya Bayern yalipachikwa na Kroos, Mueller na Mario Mandzukic huku bao la Arsenal likifundwa na mshambuliaji Lucas Podolski.
FC Porto ya Ureno ilishinda 1-0 dhidi ya Malaga katika mechi nyingine iliyochezwa hapo  jana.












 Mechi inayosubiriwa kwa hamu ni ile kati ya Barcelona na AC Milan itakayochezwa uwanja wa San Siro jijini Milan Italia. Mwaka jana kwenye michuano hii ya UEFA Barcelona na Milan zilikutana ambapo Milan walitolewa huku malalamiko mengi yakiwepo juu ya suala la mwamuzi hasa wa mechi ya marudiano kuipendelea Barcelona.
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates