NIGERIA KIDUME AFCON

SUNDAY MBA
SUPER EAGLES
 Timu ya taifa ya Nigeria hapo jana imeibuka bingwa wa AFCON 2013 shukrani kwa goli la Sunday Mba lililokatisha matumaini ya Burkinafaso kupata ubingwa katika fainali yaoya kwanza. Nigeria imepata ubingwa huo baada ya kusubiri kwa takriban miaka 19. Timu hiyo ikiwa chini ya kocha mzalendo Stephen Keshi na nyota kama Vincent Enyeama, John Obi Mikel, Victor Moses na wengine wengi imefanya vizuri ktk michuano hii tofauti na michuano mingine ya AFCON iliyopita. Burkinafaso ambayo kwa mara ya kwanza imecheza fainali za AFCON imeonyesha ukomavu na soka zuri jambo ambalo huenda likaonyesha mwanzo mzuri wa timu hiyo kwa siku zijazo
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates