Nigeria leo inacheza na Burkinafaso katika fainali ya michuano ya mataifa Afrika (AFCON) kwenye mchezo ambao huna mtabiri kutokana na matokeo ya mechi
zilizopita katika michuano hiyo.Timu zilizokuwa
zikipewa nafasi ya kunyakua taji zimeondoka patupu huku Ghana ikiambulia nafasi ya nne baada ya hapo jana kufungw 2-1 na timu ya taifa ya Mali. Timu ya taifa ya Nigeria iliyoiadhibu Mali katika mchezo wa nusu fainali leo inatarajiwa kumtumia nyota Victor Moses na Emmanuel Emenike kupata ushindi huo muhimu.Moses ambaye alikuwa majeruhi amethibitishwa kuwa yuko fiti kucheza mechi dhidi ya Burkinafso. Timu ya Nigeria hata hivyo lazima iwe makini ili wasiadhirike kama Ghana walivyofanyiwa na Burkinafaso ktk mchezo wa nusu fainali.