Home Unlabelled STURRIDGE ATUA ANFIELD
STURRIDGE ATUA ANFIELD
By burudanibuzz At January 02, 2013 0
Daniel Sturridge amekamilisha uhamisho wake kutoka Chelsea na kujiunga na majogoo wa Anfield Liverpool. Sturridge mwenye miaka 23 amekosa namba ya uhakika Chelsea na ndiyo sababu kubwa ya kuamua kutimkia Liverpool ambako kocha Brendan Rodgers ameelezea furaha yake kumsainisha mshambuliaji huyo. Wiki iliyopita Sturridge alifanyiwa vipimo vya afya kabla ya kuhamia rasmi Liverpool. Sturridge amepewa jezi namba 15 na uhamisho wake unakadiriwa kuigharimu Liver kiasi cha EURO milioni 12