Ni mwaka ambao kwa hakika umeanza vibaya baada ya Tanzania kushuhudia nyota ya mwigizaji maarufu Juma Kilowoko kufariki dunia alfajiri ya leo tarehe 2, Januari. Sajuki ambae ni mwigizaji wa muda mrefu alifariki katika hospitali ya taifa Muhimbili alikolazwa kupata matibabu baada ya afya yake kutokua ya kuridhisha kwa siku za hivi karibuni. Ikumbukwe kuwa Sajuki alitakiwa kurejea nchini India kwa ajili ya matibabu ya maradhi yaliyokua yanamsumbua ambapo Mungu ameamua kumchukua kabla. Sajuki na mke wake Wastara Juma wamepitia majaribu mengi kwani wiki chache kabla ya ndoa yao walipata ajali ya pikipiki iliyosababisha Wastara kukatwa mguu.Sajuki ameacha mke na mtoto.