NAPOLI YAMTAKA BALOTELLI, DROGBA KWENYE RADA ZA JUVE

BALOTELLI
Pamoja na uchizi na fujo zake zote huku ikiaminika ni mmoja kati ya wachezaji wasioaminika Mario Balotelli bado ana timu zinazohitaji huduma zake. Super Mario ambae maisha yake ya soka yamegubikwa na utukutu wa aina yake pamoja na kugombana na kocha wake Roberto Mancini hivi karibuni ameivutia Napoli ambapo rais wa klabu hiyo Aurelio de Laurentiis. Rais huyo anaamini Balotelli atafanya vizuri akiwa na Edinson Cavani na kuifanya timu hiyo ya Serie A kuendelea kutikisa. Aurelio alisema "My dream??Balotelli alongside Cavani in Napoli attack" na kuonesha kuwa Balotelli anaweza kupata muda mwingine wa kuacha utoto na kucheza soka.


Juventus ya Italia imeonesha kuvutiwa na mpango wa kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Didier Drogba kutoka Shanghai Shenhua. Drobga anayejiandaa na michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika (CAN) aliondoka Chelsea baada ya kuipa klabu hiyo ya London kombe la klabu bingwa Ulaya -UEFA May mwaka jana.
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates