CHRIS , FRANK OCEAN WAZICHAPA STUDIO

FRANK OCEN
BREEZY
Mwandishi na mtayarishaji wa muziki Christopher Francis Ocean "Frank Ocean" na mwanamuziki staa wa R n B Christopher Maurice Brown "Chris Brown" wameripotiwa kupigana katika studio ya Frank. Chris inadaiwa alifika katika studio hiyo kusikiliza mmoja wa wasanii anaowasimamia akifanya mambo ndani ya studio hiyo ambapo wakati wa kuondoka ndipo Frank na washikaji zake walipomzuia Chris kuondoka ambapo inasemekana Ocean aliwazuia huku akisema "This is my studio, this is my parking spot.". Baada ya hapo kilichofuatia ni ugomvi baina ya pande hizo mbili ambazao hakuna taarifa yoyoyte ya kuwepo kwa ugomvi mapema. Taarif za kipolisi zinadai kuwa hakuna hata mmoja kati ya Chris na Ocean aliyepeleka malalamiko polisi kutokana na tukio hilo.
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates