COLLOCINI VS BA |
SISSOKOAKISHANGILIA |
Klabu ya Chelsea imeshindwa kuwika ugenini mbele ya Newcastle United baada ya kutandikwa 3-2 katika uwanja wa St. James Park. Jonas Guitterez aliiweka Newcastle mbele kwa bao maridadi la kichwa katika kipindi cha kwanza, Lampard na Mata walifunga magoli mawili ya Chelsea huku Sissoko akifunga dakika ya 68 na 90 kuipa ushindi Newcastle. Mshambuliaji wa Chelsea aliyetokea Newcastle Demba Ba alikuwa na wakati mgumu kutokana na kuzomewa na mashabiki. Demba Ba alilazimika kutolewa nje baada ya kuumizwa na beki Collocini dakika ya 15 ambapo nyota huyo Msenegali aliumia vibaya pua na kumwachia Fernando Torres nafasi.