BA APIGA MBILI, VAN PERSIE MWENDO MDUNDO

DEMBA BA

RVP

Mshambuliaji mpya wa Chelsea Demba Ba ameanza vizuri maisha yake Stamford Bridge baada ya kufunga magoli mawili katika ushindi wa 5-1 dhidi ya Southampton katika kombe la FA. Hiyo ilikua mechi ya kwanza Demba Ba kucheza akiwa na jezi ya Chelsea baada ya kusajiliwa mwisho wa wiki hii akitokea Newcatle, Ba alipachika magoli katika dakika ya 35 na 61, magoli mengine yakifungwa na Ivanovic, Moses na Lampard.
Katika mechi nyingine Man U almanusra iaibshwe na West Ham kama si bao la Van Persie dakika ya 92. Man U imeambulia pointi moja kwenye hiyo mechi baada ya kupata matokeo ya 2-2 dhidi ya West Ham. Van Persie amezidi kuonyesha umuhimu wake msimu huu Man U kwa kufunga mabo mengi na anaonekana ataendelea kufanya vizuri. Brighton iliiduwaza Newcastle inayoonekana kulala na kuibuka na ushindi wa 2-0.
Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates